Burundi : Mwinjilisti Mapendo asema:’Hata kuwa walifanya makosa si wakutupwa’.
Mwinjilisti Mapendo asema:’Hata kuwa walifanya makosa si wakutupwa’.
Mapendo Anne Marie, mwanamke mwinjilisti mrundi anaeishi katika nchi ya Ubelegiji anasema kwambahata kuwa wafungwa walifanya makosa siwakutupwa kwa sababu na wale ambao hawako gerezaniwanaweza kufanya makosa kuwazidi.
Katika lengo la kuwa karibu na wale wenye matatizo, mwinjilisti Mapendo Anne Marie ameomba ruhusa maofisa wa gereza kuu la Mpimba ili kuwafikia wakaazi wa jingo hilo. Miongoni mwa wafungwa aliozungmuza nao kulikuwa na waliokuwa wanahitaji nguo, wanawake wenye mahitaji ya vifaa, Watoto watakao uji na watu ambao walikuwa na utaratibu wa matibabu lakini hawakupata uwezo wa kununua madawa.
Alipopata kibali hicho, tarehe 11 Desemba mwaka huyu , aliwakabithi wahusika wa gereza hilo misada mbalimbali kutokana na mahitaji ya wafungwa: wagonjwa 11 walilipiwa matibabu, wanawake 91 wakapatiwa pedi za usafi katika kipindi chao cha redi na Watoto kadhaa wakapatiwa nguo.
Vitambaa vya kupamba sehemu inayotumia kuomba mungu vilitolea kama anavyothibithisha mchungaji mmoja kiongozi wa waumini zaidi ya 580 wa kanisa la ECM.
Mapendo anasema kwamba kabla ya kutoa msaada huo, alikamilisha lengo lake kuu likiwa ni la kuhubilineno la Mungu. Katika mahubili yake alisaidiwa na injilisti URSULE Mulasi kutoka wa mama jeshi kubwa kutoka kanisa la Elohim church wakisaidiwa pia na muimbaji Mukengurutse Protais maarufu‘turacunzwe’(tumelindwa) anaeimba nyimbo za injili katika dini la pentekosti.Kundi la wafungwa 80 waliosaidia katika kuimba walipewa ahadi na mwinjilisti huyo ya mavaazi watakayokuwa wanayatumia wakati wa sherehe za kuomba mungu na wakibahatika kuachiliwa watayaacha mavaazi hayo gerezani kwa makusudi ya kutumiwa na wafungwa wenzao katika shuguli hiyo.
Kesho yake, akiitumia redio Voix d’Espoir,aliwaomba warundi wote kuwakumbuka wafungwa kwa sababu hata hivyo walifanya makosa si wakutupiliwa mbali . Nyuma ya wito huyo, Mapendo alithibitishakwamba kuna watu wanaojitolea kwa wingi wakitowa biblia au vyakula na anawashuru sana akindelea kuwaomba warundi wawasaidie wafungwa kwa sababu na wao ni viumbe.
Nyuma ya mikutano ya maombi na neema, watu wengi waliohudhulia waliokoka hasa wale waliokuwa wakifanya punyeto . Mapendo akishukuru sana kazi ya mungu na kutuguliwa roho na hali ya wafungwa katika magereza.
Ikumbukwe kwamba mwinjilisti Mapendo Anne Marie alipita anaelekea nchini Tanzania kuhubili na tayari amesha rudi Burundi akijiandaa kuelekea nchini Malawi katika kazi hiyo hiyo.